Duration 56:29

Pd Kamugisha Awasili DSM/Vicheko vyatawala Parokia ya Kilongawima/Karama aliyo nayo siyo ya kawaida.

30 581 watched
0
173
Published 4 Nov 2021

Tarehe 01 November 2021 Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu katoliki la Dar Es Salaam Mhasham Henry Mchamungu Aliongoza Ibada ya Uzinduzi wa Wiki mbili za Neema katika Parokia ya Mtakatifu kizito Kilongawima Mbezi Jijini Dar Es salaam Ambapo alimpongeza Paroko wa Parokia hiyo Padre Mukandala kwa maandalizi mazuri ya kuwalisha neno la Mungu waamini wa Parokia yake kwa kuwakusanya zaidi ya Mapadre 15 kutoka majimbo mbalimbali ya Tanzania ambao ndio watakaotoa Mafunzo kwa waamini hao. Semina hiyo ya wiki mbili za Neema imeanza kurindima tarehe 02/11/2021 katika viwanja vya Parokia hiyo na Miongoni mwa Mapadre ambao wamekuwa wa kwanza kabisa kutoa mafundisho ni Padre Novatus Mbaula kutoka Msimbazi Centre Dar es salaam huku akifuatiwa na Padre Faustine Kamugisha kutoka Parokia ya Minziro jimbo katoliki la Bukoba. Waamini wengi waliofika katika Siku ya kwanza ya mafundisho hayo wengi wao wameonekana kujawa na Tabasamu mwanana mara baada ya Wakufunzi hao kuwalisha Chakula cha kiroho huku wengi wao wakieleza kuwa, ni wazi wale ambao hawajashiriki wanakosa mengi ikiwemo faraja ya kweli ambayo inawarudisha katika imani dhabiti pamoja na kuimarika zaidi ndani ya Ubatizo wao. pata nafasi ya kutazama video hii na kuwa miongoni mwa wale ambao wamefuatilia Mubashara. #BreezOnlineTv​​​​​​​​​​​​​ #Kilongawima Breez Online Tv S.L.P 38655 Dar Es Salaam Tanzania Phone No: +255 756494796 Barua pepe: izackbreez11@gmail.com Mitandao Mingine ya Kijamii: Facebook: breez online Tv Facebook Link: https://www.facebook.com/Breez-Online ... Instagram:Breez Online Tv

Category

Show more

Comments - 31
  • @
    @saulokahwa81944 months ago Tunabarikiwa na mafundisho yako baba ubarikiwe sana
  • @
    @gidionmibaluro70853 months ago kwakweli tunazid kubalikiwa.......Mungu azid kushusha neema yake
  • @
    @ceciliamasawe75663 years ago Tunabarikiwa Sana na mahubiri yako Mungu akubariki! Karibu sana parokia ya Mt Gaudes Makoka 2
  • @
    @benedictodaud7769last year Tyk.baba kamgisha.napenda sana mafundisho yako.mungu akubariki sana.Napenda siku moja uje parokian kwetu,dsm parokia ya mt,marther mikocheni (b)
  • @
    @amedeusmushi13573 years ago Ubarikiwe sana baba padre nimependa iyo kuvuruga kiota hakuna kulea tuu 1
  • @
    @anneduncan48363 years ago Napenda sana mafundisho yako yananipa nguvu na faraja mno nimesikitika. Sikujua kama ulikuja Dar nisingekosa 1
  • @
    @NiyomugenziAime-gc3hx6 months ago Fundi wa mafunzo,Fundi wa faraja, Fundi wa ufafanuzi Padre Kamgisha Mungu Azidi Kukubariki na Kukulinda
  • @
    @ghatimakonge93833 years ago Nakupenda kwa MOYO wa dhati ❤️ father kamgisha karibu Parokia ya Mt Rafael malaika mkuu nyamongo utupe vitu adimu vilivyomo Ktk Ubongo wako.🙏🙏🙏🙏🙏🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🙏🔥🔥 3
  • @
    @EdinaMashongole2 months ago Nimekulewa vuruga kiota.mbavu zangu jamani
  • @
    @julianacellestine8013 years ago Asante father neno lako lenye kujenga ubarikiwe sana na Mungu wa mbinguni akubariki sanaaa
  • @
    @jaqualineobuchi22563 years ago Asante padri mungu azidi kukubariki kwa kazi yako njema. 2
  • @
    @eliaskangabo7796 months ago Baba Mungu akubariki kwa mahubiri. Yako Mungu Skype maisha marefu
  • @
    @mkudembeteni76673 years ago Wakati ujao mtakapo jaaliwa kumketa Father Kamugisha Mtupe taarifa rasmi tuna shauku kubwa Sana ya kumuona huyu mtumishi 1
  • @
    @mucoluckyjob-love37843 years ago huu padri anakipaji kbs yani wa padri wote wangekua kama huu watuwengi wangekua nahamu yakwenda kanisani 😁 kwasababu hiyo mifano yake kama anaisomaka wapi