Duration 9:45

Taasisi ya Muzdalifa watoa msaada wa magodoro 100 kwa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar

367 watched
0
6
Published 24 Sep 2021

Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Khamis Bakari Khamis amepokea msaada wa magodoro mia moja kutoka kwa Taasisi ya Muzdalifa na Mtandao wa Haki za Binaadamu Tanzania THRDS kwa ajili ya Wanafunzi wanaotumikia kifungo Chuo cha Mafunzo . Akipokea msaada huo makao makuu ya Chuo cha Mafunzo Kilimani, Kamishna Khamis amezishukuru taasisi hizo kwa kuona umuhimu kuimarisha mazingira mazuri kwa wanafunzi hao ambao wanauhitaji mkubwa katika kuwarekebisha tabia ili kuwa raia wema hapo baadae . ‘‘Tunatoa wito kwa NGO’s nyengine wasisite kutoa misaada tofauti kwa ajili ya Wanafunzi wetu wa Chuo cha Mafunzo kwa vile uhitaji upo mwingi wa Wanafunzi hao" alisema. Nae Mkurugenzi wa Muzdalifa Charitable Organisation Farouk Hamad Khamis amesema kuwa taasisi imehamasika kutoa msaada huo kupitia michango ya wafanyakazi pekee ,kwa ajili ya kuiunga mkono Serikali kwa kuweka mazingira bora kwa wanafunzi. Kwa upande wake Afisa mkuu wa taasisi ya mtandao wa haki za binaadamu Tanzania, Onesmo Olengurumwa, amesema kuwa wataimarisha ushirikiano na Serikali katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kibinaadamu. . Ameongeza kuwa wanafunzi waliopo kifungoni wanakuwa na uhitaji mkubwa na hawana uwezo wa kutoka kutafuta haki zao za msingi, hivyo kama ni taasisi imeona umuhimu wa kuwasidia ingawa wapo katika kurekeshishwa tabia.

Category

Show more

Comments - 0