Duration 2:38

WATU WASIOJULIKANA WACHOMA NYUMBA KIBAHA “MMOJA AMEUNGUA NA KUFARIKI, ZUWENA ALIWAITISHIA WIZI”

5 334 watched
0
28
Published 26 May 2021

Mkazi wa Umwerani, Kata ya Kongowe, Kibaha Mkoani Pwani Mrisho Omary amefariki baada ya nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi kuchomwa moto na Watu wasiojulikana akiwa amelala na wenzake ndani. Watu wengine waliokuwa kwenye nyumba hiyo siku ya tukio May 15,201 ni Mwalimu Ally Shaban na Lusekelo ambapo wote waliwaishwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi na Mrisho akafariki May 17. “Mwanamke mmoja anaitwa Zuwena alipiga kelele akisema amebakwa na kuibiwa simu na Elfu 30 na Watu hao watatu, Watu hao wakakimbilia kwenye nyumba hiyo ndipo Wananchi wenye hasira kali wakaichoma nyumba moto”———RPC Pwani, Wakyo Nyigesa “Uchunguzi wa awali unaonesha kulikuwa na ugomvi wa kimapenzi kati ya Zuwena na Watu hao aliowaitishia wizi na upelelezi unaendelea kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo”———-RPC Pwani #MillardAyoUPDATES

Category

Show more

Comments - 36